ĂŰĚŇ˝»ÓŃ

Nembo ya UNICEF. Nembo ya UNICEF. 

UNICEF:Watoto milioni 213 wanakabiliwa na dharura za kibinadamu,Ulimwenguni

UNICEF imezindua Ripoti yake mpya ya Majibu ya Kibinadamu yenye ombi la kuchangisha fedha la dola bilioni 9.9 ili kufikia watoto milioni 109 katika nchi 146 kwa msaada wa kuokoa maisha mwaka wa 2025.Fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kukabiliana na UNICEF ya kibinadamu inasema migogoro mingi,majanga ya tabianchi na kuyahama makazi yao na majanga ya kiafya yanatarajiwa mwaka ujao.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ulimwenguni kote, watoto milioni 213 wanakabiliwa na dharura za kibinadamu zisizotabirika na zinazobadilika kila wakati. Huku ikiwa na watoto milioni 109 ambao UNICEF inawapangia msaada wa kibinadamu mwaka 2025, ufadhili wa kifadhili ni muhimu ili kuhakikisha mwitikio huo unapatikana kwa wakati, thabiti na wa kutosha. Hayo yamethibitishwa na Ripoti mpya iliyozinduliwa na UNICEF tarehe 5 Desemba 2024. "Kiwango cha mahitaji ya kibinadamu ya watoto kiko katika kiwango cha juu kihistoria, huku watoto wengi wakiathirika kila siku," Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF,  Bi Catherine Russell alisema. "Tukiangalia mbele hadi 2025, tunakadiria kuwa watoto milioni 213 katika nchi na wilaya 146 watahitaji usaidizi wa kibinadamu katika kipindi cha mwaka - idadi kubwa. Ni kazi ya UNICEF kufikia kila mmoja wa watoto hawa na huduma muhimu na vifaa wanavyohitaji, na kuhakikisha kwamba haki zao zinalindwa na kuzingatiwa – jukumu ambalo limeongoza kazi yetu kwa miaka 78 iliyopita.”

Milioni 57.5 ya watoto wamezaliwa katika nchi za migogoro

Zaidi ya hayo, mnamo 2024, zaidi ya watoto milioni 57.5 walizaliwa katika nchi zilizoathiriwa na migogoro au machafuko mengine ya kibinadamu ambapo UNICEF ilitoa rufaa ya dharura. Idadi hii inatarajiwa kuongezeka kwa angalau vitengo 400,000 katika 2025. Wito kwa ajili ya  dola bilioni 9.9 kwa mwaka 2025 inaakisi  hitaji la dharura la kukabiliana na changamoto zinazoongezeka za kibinadamu zinazowakabili watoto katika nchi 146. Mwaka 2023 wafadhili walichangia zaidi ya 50% ya ufadhili wa kimaudhui wa UNICEF katika dharura nne tu - Afghanistan, Ethiopia, Syria na Ukraine - sehemu ya dharura 412 ambazo UNICEF ilijibu katika nchi 107.

Nchi nyingine zinazokosa fedha

Unicef aidha inabainisha kuwa wakati huo huo, oparesheni za kibinadamu katika nchi kama vile Burkina Faso, Lebanon, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,(DRC) Mali na Myanmar zimekuwa zikikosa fedha nyingi zaidi. "Kusaidia rasilimali za kibinadamu za UNICEF zinazobadilika na kutoka ngazi ya chini ni muhimu kwa kazi yetu na watoto walioathiriwa na majanga," Russell alisema. "Fikiria kile tunachoweza kufikia kwa watoto kwa kufanya kazi pamoja kupitia hatua za maana za kibinadamu, kuunda ulimwengu ambapo haki za kila mtoto zinalindwa na kuungwa mkono, na ambapo kila mtoto anaweza kukua na kustawi - ulimwengu ambao unafaa kila mtoto".

05 December 2024, 17:38