ĂŰĚŇ˝»ÓŃ

Trum ameshinda tena urais wa Marekani. Trum ameshinda tena urais wa Marekani. 

Ushindi wa Trump kwa mhula mwingine wa urais nchini Marekani

Katika mbio za marathoni za uchaguzi za Marekani rais wa zamani alimshinda Kamala Harris,na kurejeshwa Ikulu baada ya mamlaka yake yaliyofanyika kati ya 2017 na 2021.Donald Trump,mwenye umri wa miaka 78,ndiye wa kwanza kuhudumu mihula miwili ya urais bila mfululizo na rais mzee zaidi kuchukua madaraka.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Donald Trump kwa mara nyingine tena ni rais wa 47 wa Marekani. Tangazo la mshindi lilizinduliwa kwa mara ya kwanza na kipindi cha televisheni cha Marekani Fox News, tangazo hilo rasmi lilikuja baada ya uthibitisho pia kurekodiwa katika Jimbo la Wisconsin ambalo lilimfanya kuzidi kiwango cha wapiga kura 270 wanaohitajika. Mpinzani, Kamala Harris, alishinda katika majimbo 18.

Hotuba kwa wafuasi

Katika hotuba yake ya ushindi kutoka Palm Beach kwa wafuasi wake waliokusanyika katika Kituo cha Mikutano, Trump alibainisha kwamba atatimiza ahadi zake, kuanzia kukata kodi na kupunguza deni la shirikisho la Marekani. “Kazi inayotungoja haitakuwa rahisi - aliongeza - lakini nitaweka kila chembe ya nguvu, ari na dhamira katika kukamilisha kazi uliyonikabidhi. Itakuwa enzi mpya ya dhahabu.”  Kisha aliongeza: “Sitaanzisha vita, lakini nitavikomesha.” Bi Kamala Harris, wakati wa usiku, baada ya kuwasili kwa takwimu  nyingi kwa ajili ya mpinzani wake, aliacha “makao makuu” yake.

Trump kuelekea kwa muhula wa pili

Donald Trump, mwenye umri wa miaka 78, ndiye wa kwanza kuhudumu mihula miwili ya urais bila mfululizo na rais mzee zaidi kuchukua madaraka. Kazi yake ya kisiasa inachukuliwa kuwa kazi ambayo haijawahi kushuhudiwa kwani alifanikiwa kurejea Ikulu kupitia mashtaka mawili, mashitaka mbalimbali na makosa mawili ya jinai. Baada ya shambulio la Capitol Hill, mwelekeo wake wa kushuka ulionekana dhahiri, ukiwa umeachwa hata na chama chake, ambacho alifanikiwa kupata tena.

Mwitikio wa jumuiya ya kimataifa

Hata hivi ujumbe mwingu wa pongezi umemiminika kwa Donald Trump kutoka  ulimwenguni kote. “Tuko tayari kufanya kazi pamoja kwani tumeweza kufanya hivyo kwa miaka minne. Kwa amani na ustawi zaidi,” rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, aliandika kwenye X. Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alifafanua ushindi wa Trump kama “kurejea kubwa zaidi katika historia.” Kutoka kwa Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, ujumbe wa hamu ya kuendeleza ushirikiano katika kile alichofafanua kama “muungano usioweza kutetereka, na maadili ya kawaida na urafiki wa kihistoria.” Volodymyr Zelensky, alimpongeza Trump kwa “ushindi wake wa kuvutia”, akitumaini kuwa kama rais wa Marekani “ataisaidia Ukraine kufikia amani ya haki.”

Ushindi wa Trump
07 November 2024, 10:08