ҽ

Mkutano wa Tabianchi COP29 huko Baku Mkutano wa Tabianchi COP29 huko Baku 

COP29:Taasisi 27 za kidini,vikao vilivyofanyika 28 hadi sasa havikubadili mwelekeo wa kukomesha hewa chafuzi

Katika taarifa iliyotolewa na Taasisi 27 za kidini kimataifa kuhusiana na Mkutano wa UN wa COP29 uliofunguliwa huko Baku tarehe 11 Novemba 2024,zibainisha kuwa kuwekeza katika nishati ya kisukuku sio maadili tena mbele ya athari mbaya za hali yatabianchi,viumbe hai na ubinadamu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumanne tarehe 12 Novemba 2024,  taasisi 27 za kidini zimetangaza kutowekeza kwenye makampuni ya mafuta na kutuma wito mkali  kwa washiriki  wa COP29, katika mkutano wa Umoja wa Mataifa wa tabianchi unaendelea huko  Baku nchini Azerbaijan kuanzia tarehe 11 hadi 22 Novemba 2024. Katika taarifa ya pamoja ya Movimento Laudato si',(Harakati za Laudato Si) –Operation Noah,(Operesheni ya Noah) World Council of Churches,(Baraza la Makanisa Ulimwenguni) Green Anglicans (Waanglikani wa Kijani) na GreenFaith(Imani ya kijani) zinaibainisha kwamba hazikubaliki kiadili, kwa kuzingatia athari mbaya ya uchimbaji na uchomaji wa nishati ya kisukuku kwenye hali ya hewa, tabanchi,  bioanuwai na haki za binadamu. Wakati uzalishaji wa gesi chafuzi unaongezeka kwa kasi zaidi kuliko wakati wowote katika historia ya binadamu na matukio mabaya ya hali ya tabianchi  kama vile mafuriko mabaya ya mwezi uliopita nchini Hispania yanazidi kuwa ya kawaida, viongozi wa kidini wanajali sana kuhusu kuendelea makampuni ya mafuta kuendelea kuwekeza katika nishati ya joto ya sayari na mipango ya kupanua uzalishaji, hasa wakati nishati safi, nafuu, na nyingi zaidi inapatikana katika mfumo wa nishati ya jua na upepo.”

Kampeni ya tabiachi 

“Zaidi ya miaka kumi ya kampeni ya tabianchi ya kidini, zaidi ya taasisi za kidini 570 ulimwenguni kote zimejitolea kuachana na nishati ya mafuta, pamoja na Mipango  ya Kitaifa ya Uwekezaji ya Kanisa la Uingereza, Wajesuit huko Uingereza, Canada, Australia na Jimbo la Mediterania la Ulaya, Kanisa la Sweden na Kanisa la Kianglikani la Kusini mwa Afrika”, inakumbukwa na kuongeza kuwa "orodha ya leo  hii ya taasisi ambazo zimeamua kuachana nazo ni pamoja na majimbo kumi na moja ya Kikatoliki (nane nchini Italia, mawili Ufaransa na moja Ireland), madshirika tisa ya kidini ya Kikatoliki, majimbo mawili ya Kanisa la Uingereza, Chuo Kikuu kimoja cha Kikatoliki nchini Canada na Vyama vya Kikristo vya Wafanyakazi wa Italia.” Nchini Italia, pamoja na Acli, majimbo ambayo yanatangaza kutowekeza, ishara ya kuongezeka kwa msimamo wa Kanisa Katoliki kwa kuondoka kutoka kwa nishati ya mafuta, ni yale ya Acireale, Chioggia, Cuneo-Fossano, Locri-Gerace, Pinerolo, Porto-Santa Rufina na Mileto-Nicotera-Tropea.

Uwekezaji mkubwa wa taasisi za kidini

 Katika taarifa hiyo inasisitiza kuwa -"Taasisi za kidini  husimamia jumla ya dola bilioni 3,000 katika uwekezaji duniani kote na, kwa kuoanisha maadili yao na uwekezaji wao, wameondoa kutoka kwa nishati ya mafuta zaidi ya sekta nyingine yoyote. Vatican na Baraza la Makanisa Ulimwenguni (WWC)  wametoa wito kwa vikundi vya kidini kutoa pesa zao kutoka katika kampuni za mafuta - kulingana na makadirio fulani, kampuni za mafuta hutumia wastani wa 5% tu ya mtaji wao uliowekeza kwenye nishati mbadala na uzalishaji mdogo wa hewa chafuzi  na  badala yake kuwekeza katika ufumbuzi wa hali ya hewa.

Vikao 28 vilivyofanyika hadi sasa havikuweza kutoa kabisa hewa chafuzi

Katika kipindi cha miaka 10, zaidi ya taasisi 1,600 katika sekta zote, pamoja na mali ya zaidi ya $40 trilioni, zimetoa ahadi ya uondoaji wa mafuta, kutoka mwanzo wa $50 bilioni mwaka 2014. Mbali na kutowekeza, jumuiya za kidini pia zinatoa wito kwa serikali na benki kuacha msaada wao kwa nishati ya mafuta na kuongeza uwekezaji katika nishati safi, na vikundi zaidi vya imani vinavyowekeza katika ufumbuzi wa hali ya hewa wenyewe. Kulingana na mashirika yaliyotia saini, "kutelekezwa kwa nishati ya mafuta na taasisi za kidini kunatoa ishara kali kwa serikali za kitaifa wakati wa Cop29, mazungumzo ya hali ya tabianchi yaliyokuzwa na Umoja wa Mataifa" pia kwa sababu "Katika vikao 28 vilivyotangulia, ambavyo mara nyingi viliathiriwa sana na mataifa ya mafuta na makampuni ya mafuta, viongozi wa kimataifa walizungumza hadharani lakini walishindwa kubadili mwelekeo wa utoaji wa hewa chafuzi.

Taasisi 27 za Kidini kutoa wito katika COP29
12 November 2024, 11:08