ҽ

Juma la  Kimataifa ya Upokonyaji Silaha ya Umoja wa Mataifa inalenga kukuza ufahamu na uelewa bora wa masuala ya upokonyaji silaha na umuhimu wake mtambuka. Juma la Kimataifa ya Upokonyaji Silaha ya Umoja wa Mataifa inalenga kukuza ufahamu na uelewa bora wa masuala ya upokonyaji silaha na umuhimu wake mtambuka.  (ANSA)

Juma la Kimataifa la UN la Upokonyaji wa Silaha 24-30 Oktoba 2024!

Uchaguzi na sera za upokonyaji silaha hufuatwa kwa sababu nyingi,ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na usalama wa kimataifa,kuzingatia kanuni za ubinadamu,kulinda raia,kukuza maendeleo endelevu,kukuza uaminifu kati ya Mataifa na kuzuia na kukomesha migogoro ya silaha.Haya ni katika jukumu la Juma la Kimataifa la UN la Upokonyaji silaha 24-30 Oktoba 2024.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Juma la Upokonyaji Silaha unaoendelezwa na Umoja wa Mataifa(UN) kwa mwaka 2024 linaongozwa na mada: Tunahitaji kufuata Ajenda ya Kupokonya Silaha ya kweli ili kujenga jamii yenye amani, inayotokana na Kutonyanyasa. Kwa hiyo ni muhimu kuzindua upya mapendekezo ya kupunguza kuenea kwa silaha, kupiga marufuku mifumo hatari zaidi ya silaha na kuhimiza uhamisho wa rasilimali kutoka katika matumizi ya kijeshi ili kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu na kushughulikia dharura ya afya na hali ya tabianchi. Ili kusherehekea kumbukumbu ya miaka hii(iliyoanzishwa  na Umoja wa Mataifa pia kubaki katika historia yake, ambayo ilianza na azimio rasmi la kwanza lililopigwa kura juu ya mada ya uondoaji wa silaha za nyuklia) kuna mipango mbalimbali na muhimu pia iliyokuzwa na “Mtandao wa Amani bila silaha”  katika juma zima.

Azimio la UN mnamo 1995

Ikumbukwe Juma la Kimataifa ya Upokonyaji Silaha la Umoja wa Mataifa linalenga kukuza ufahamu na uelewa bora wa masuala ya upokonyaji silaha na umuhimu wake mtambuka. Kuanzia tarehe 24 Oktoba, ukumbusho wa kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, maadhimisho ya kila mwaka ya juma yalitolewa kwa mara ya kwanza katika hati ya matokeo ya kikao maalum cha Baraza Kuu la 1978 kuhusu upokonyaji silaha (azimio S-10/2). Mnamo 1995, Baraza Kuu lilitoa wito kwa serikali, pamoja na Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGOs), kuendelea kushiriki kikamilifu katika Juma la Upokonyaji Silaha (azimio la 50/72 B, 12 Desemba 1995) ili kukuza uelewa mzuri wa umma wa masuala ya upokonyaji silaha. Katika historia, nchi zimefuata upokonyaji silaha ili kujenga ulimwengu salama na kulinda watu dhidi ya vitisho na athari mbaya.

Mlundikano wa kupindukia wa biashara haramu ya silaha

Tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, upokonyaji silaha na udhibiti wa silaha umekuwa na jukumu muhimu katika kuzuia na kumaliza migogoro na mitatizo ya silaha. Mivutano inayoongezeka na hatari hutatuliwa vyema kupitia mazungumzo na mazungumzo mazito ya kisiasa, na sio kwa silaha zaidi. Silaha za maangamizi makubwa, hasa silaha za nyuklia, zinaendelea kuwa jambo la msingi, kutokana na nguvu zao za uharibifu na tishio zinazoleta kwa wanadamu. Mlundikano wa kupindukia na biashara haramu ya silaha za kawaida unahatarisha amani na usalama wa kimataifa na maendeleo endelevu, huku matumizi ya silaha nzito za kawaida katika maeneo yenye watu wengi yanahatarisha pakubwa raia.

Teknolojia mpya zinazoibuka za silaha ni hatari kwa usalama wa kimataifa

Teknolojia mpya na zinazoibukia za silaha, kama vile silaha zinazojiendesha, zinahatarisha usalama wa kimataifa na zimepokea umakini mkubwa kutoka katika jumuiya ya kimataifa katika miaka ya hivi karibuni. Uchaguzi na sera za upokonyaji silaha hufuatwa kwa sababu nyingi, ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na usalama wa kimataifa, kuzingatia kanuni za ubinadamu, kulinda raia, kukuza maendeleo endelevu, kukuza uaminifu kati ya Mataifa, na kuzuia na kukomesha migogoro ya silaha. Hatua za upokonyaji silaha na udhibiti wa silaha husaidia kuhakikisha usalama wa kimataifa na binadamu katika karne ya 21 na kwa hivyo lazima ziwe sehemu muhimu ya mfumo wa usalama wa pamoja unaoaminika na madhubuti.

UN kuendeleza juhudi za ushiriki wa mstakabali wa usalama na amani 

Umoja wa Mataifa unaendelea kupongeza juhudi na ushiriki wa wahusika mbalimbali wanaochangia mustakabali wa pamoja ulio salama na wenye amani kupitia upokonyaji silaha, udhibiti wa silaha na juhudi za kutosambaza silaha. Katika ulimwengu unaotishiwa na silaha za maangamizi makubwa, silaha za kawaida na vita vya mtandao vinavyoibuka, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres aliwasilisha ajenda mpya ya upokonyaji silaha mnamo  mwaka 2018 ili "kuokoa ubinadamu, kuokoa maisha na kulinda mustakabali wetu wa pamoja."

Siku za Umoja wa Mataifa la Upokonyonyaji wa silaha 24-30 OKTOBA 2024
25 October 2024, 14:06