ҽ

Siku ya Unene Duniani inaadhimishwa kila tareh 4 Machi ya kila mwaka. Siku ya Unene Duniani inaadhimishwa kila tareh 4 Machi ya kila mwaka. 

Siku ya Unene Duniani: Watoto milioni 37 chini ya miaka 5 wameathiriwa na uzito kupita kiasi

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Hali ya Watoto katika Umoja wa Ulaya, matukio ya unene na uzito kupita kiasi yamekuwa ya wasiwasi mkubwa ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na duniani kote.Katika bara la Ulaya ya Kusini mnamo 2022 kulikuwa na watoto 500,000 waliokuwa na uzito kupita kiasi,sawa na 8.3% ya watoto chini ya miaka 5.

Na Angella Rwezula - Vatican.

Katika maadhimisho ya Siku ya Kunenepa Duniani iadhimishwayo kila ifikapo tarehe 4  Machi 4, UNICEF inakumbusha kuwa inakadiriwa  mwaka 2022, watoto milioni 37 walio chini ya umri wa miaka 5 waliathiriwa na unene uliopitiliza duniani, yaani 5.6% ya jumla. Kulingana na ripoti hiyo inaonesha mwelekeo wa utapiamlo wa watoto, makadirio ya pamoja ya utapiamlo wa watoto yaliyotolewa na UNICEF, WHO na Kundi la Benki ya Dunia, barani Asia kulikuwa na watoto milioni 17.7 chini ya umri wa miaka 5 ambao walikuwa na uzito kupita kiasi, barani Afrika milioni 10.2, kwa Amerika Kusini na Carribien 4.2, Ulaya milioni 2.6, katika bara ka Ocean milioni 0.2. Katika nchi za kipato cha juu na cha kati, ambapo 31% ya watoto wote duniani chini ya umri wa miaka 5 wanaishi, 48% ya watoto wote walioathiriwa na uzito mkubwa wamejilimbikizia. Katika bara la Ulaya ya Kusini mnamo 2022 kulikuwa na watoto 500,000 waliokuwa na uzito kupita kiasi, sawa na 8.3% ya watoto chini ya miaka 5.

Matukio ya unene na uzito kupita kiasi

Kulingana na ripoti ya hivi karibuni ya Hali ya Watoto katika Umoja wa Ulaya, matukio ya unene na uzito kupita kiasi yamekuwa ya wasiwasi mkubwa ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na duniani kote. Kadirio la viwango vya watoto na vijana walio na uzito uliopitiliza/unene kupita kiasi na vijana walio na umri wa hadi miaka 19 mwaka wa 2019 walikuwa ni kati ya 20-25% nchini Estonia, Latvia na Lithuania hadi karibu 40% nchini Syaprus na Ugiriki. Italia ilikuwa katika nafasi ya 4 katika Umoja wa Ulaya kati ya walioathirika zaidi, na asilimia ya karibu 36% kwa wasichana na 43% kwa wavulana.

Mamilioni ya watoto  wanakula vyakula visivyo faa

Lishe ya kutosha ni haki ya msingi ya binadamu kwa kila mtoto na njia ya maisha bora ya baadaye. Kwa bahati mbaya, mazingira ya chakula ambayo mamilioni ya watoto wanaishi leo yanawakilisha tishio linaloongezeka kwa afya na ustawi wao. Mamilioni ya watoto leo hii wanakula sana vyakula visivyofaa. Hii inachangia ongezeko la haraka la uzito mkubwa kwa watoto, na kusababisha matatizo makubwa ya afya ya muda mrefu. Mabadiliko mabaya ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika mazingira ya chakula cha watoto - mahali wanapoishi, kujifunza, kucheza na kula - yanachochea mienendo hii. Kwa upatikanaji rahisi wa vyakula visivyo na afya, vya bei ya chini, watoto - hasa wale walio katika umaskini - hawapati lishe bora wanayohitaji kwa ukuaji wa afya.

Unene kupita kiasi unaleta hata kunyanyapaa

Uuzaji wa vyakula vilivyonyonywa na usiodhibitiwa una jukumu kubwa katika shida hii na inahusishwa moja kwa moja na kuongezeka kwa uzito kupita kiasi, unene na afya mbaya kwa watoto. Inawafikia watoto kupitia utangazaji wa magazeti, televisheni na nafasi za mtandaoni. Tuna fursa ya kubadilisha mifumo ya chakula na kuhakikisha watoto wote, bila kujali wanaishi wapi, wanapata ufikiaji sawa wa chaguo bora zaidi za afya na lishe zaidi ambazo zinasaidia ustawi wao wa kimwili na kiakili. Muhimu sawa ni hitaji la kufungua mazungumzo ya huruma juu ya uzito kupita kiasi na unene. Hata hivyo “Kuwalaumu watu binafsi kwa uzito wao hakuna tija na kunaweza kuathiri vibaya afya ya kihisia na kimwili ya watoto wanaoishi na uzito kupita kiasi na unene kupita kiasi. Unene uliokithiri utotoni unazidi kuhusishwa na unyanyasaji na unyanyapaa, jambo ambalo huweka mkazo katika afya ya akili ya watoto na kuwakatisha tamaa kufuata mazoea yenye afya. Lazima tufanye kila tuwezalo kukuza mazingira wezeshi na kutafuta njia za kupunguza unene.”

04 March 2024, 11:47