Misri,wahamiaji wa Sudan wafariki kwenye gari
Pope
Waathirika wa wahamiaji sio tu wa baharini lakini pia hata njia za ardhini pia hupoteza maisha. Nchini Misri, hivi karibuni, tarehe 21 Februari 2024 watu 11 walifariki kwenye lori wakitokea nchini Sudan. Gari hilo lilipinduka na kuwaka moto, ambapo hakuweza kumbia abiria waliokuwa wamekwama ndani humo. Watu wengine 6 waliojeruhiwa walihamishiwa hospitalini. Wahusika wakuu wa ajali hiyo iliyotokea kwenye barabara ya Al-Alaqi mjini Aswan, walikuwa wahamiaji wakitokea Sudan.
Zaidi ya Milioni 1.7 ya wakimbizi wa Sudan wako Sudan Kusini,Chad,Ethiopia,Afrika ya Kati na Libya
Mamlaka za eneo hilo zinachunguza tukio hilo na wamefungua kesi. Lakini hii inaonekana kuwa sehemu nyingine katika muktadha wa kile ambacho, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ni mojawapo ya wahamiaji wakubwa zaidi katika sayari kutokana na vita vikali vinavyoikumba Sudan na ambavyo mashirika mengi yanatoa wito wa kusitishwa kwa haraka mapigano na kuna zaidi ya wakimbizi milioni 7 na watu elfu 700 wamekimbia hadi sasa tangu mwanzoni mwa mwaka 2024 na ambao, kwa sehemu, wamevuka mipaka ya Misri. Zaidi ya milioni 1.7 pia wamekimbilia makazi yao Sudan Kusini, Chad, Ethiopia, Afrika ya Kati na Libya.