Papa amefanya Uteuzi wa Maaskofu wawili Polvani na Cimpanelli katika taasisi za Vatican
Pope
Baba Mtakatifu Francisko amefanya iteuzi mara mbili mjini Vatican tarehe 12 Januari 2025 ambao kwanza ni Monsinyo Carlo Maria Polvani, aliyekuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Utamaduni na Elimu Katoliki, kushika nafasi ya Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, pamoja na kupewa wadhifa wa Regie, kama Askofu mkuu. Wakati huo huo Papa Francisko amemteua Monsinyo Filippo Ciampanelli, kuwa Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki na kumteua kuwa Askofu na kiti cha heshima cha Acque ya Mauritania.
Monsinyo Carlo Maria Polvani alizaliwa Milano nchini Italia mnamo tarehe 28 Julai 1965. Alihudhuria Mafunzo katika Taaasisi ya Leone XIII huko (Milano) na Chuo cha Stanislas (Montréal) ambapo alihitimu katika Biokemia na kupokea udaktari wake. Elimu yake pia ni pamoja na Shahada ya Uzamili wa Taalimungu katika Chuo cha Taalimungu cha Weston Jesuit (Cambridge, Marekani), Mhitimu wa Leseni katika Sheria za Kanisa kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregoriani, taaluma ya Sheria na Saikolojia ya Uchunguzi na Shahada ya Uzamivu katika Sheria za Kanoni. Tangu mwaka 2013 amekuwa Mhusika wa Heshima wa Papa. Alikuwa Balozi huko Mexico. Tangu 2001 amefanya kazi katika Sekretarieti ya Vatican kama mkuu wa Ofisi ya Habari na Nyaraka na Ofisi ya Kiufundi ya Sehemu ya Masuala ya Jumla, pamoja na mwakilishi wa Vatican katika Kamati ya Ushauri ya Serikali ya Shirika la Mtandao kwa Majina Yaliyokabidhiwa na Idadi (ICANN). Kunako mwaka 2015 aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Vyombo vya Habari vya Vatican na wa Kamati Tendaji ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya Vatican.
Katibu Msaidizi wa Baraza la Kipapa la Makanisa ya mashariki
Monsinyo Filippo Ciampanelli, alizaliwa huko Novara Italia na alihudumu katika NUbalozi huko Georgia, Armenia, Azerbaijan na Belarus. Akiwa na Shahada ya Uzamivu ya Taalimungu kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Gregorian, amekuwa akihudumu katika Sehemu ya Masuala ya Jumla ya Sekretarieti ya Vatican tangu 2015. Papa Francisko , katika hali ya kutowezekana, mara nyingi amemtegemea yeye kusoma hotuba zake.