Ask.Mkuu Gallagher yuko safarini huko Jamhuri ya Congo
Pope
Ni safari ya kuelekea Jamhuri ya Congo ya Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Vatican anayeshughulikia Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa, kuanzia Jumamosi tarehe 11 Januari na kuendelea hadi Jumanne tarehe 14 Januari 2025. Fursa ya safari hiyo ni mwanzo wa kazi ya Tume ya Pamoja ya utekelezaji wa Mkataba wa Mfumo, uliotiwa saini mnamo 2017 na kuanza kutumika mnamo 2019.
Mpango wa ratiba ya safari yake
Kwa mujibu wa programu iliyotolewa na akaunti ya X ya Sekretarieti ya Vatican @TerzaLoggia, inabainisha kuwa kituo cha kwanza nchini humo kitakuwa ni ziara ya tarehe 12 Januari kwenye kaburi la Mtumishi wa Mungu, Kardinali Emile Biayenda katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu. Baadaye Askofu Mkuu Gallagher ataadhimisha Ibada ya Misa Takatifu katika fursa ya Jubulei ya Harakati ya Kitume katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Maria. Utafuatia Mkutano na maaskofu wa Congo.
13/14 Januari
Siku itakayofuata,yaani 13 Januari 2025, Askofu Mkuu atafanya ziara ya heshima kwa Rais wa Jamhuri,ya Congo, Bwana Denis Sassou N'Guesso, na kisha kwa Waziri Mkuu, Anatole Collinet Makosso. Baadaye atakutana na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje Bwana Jean-Claude Gakosso. Sherehe ya uzinduzi wa kazi ya Tume ya Pamoja ya utekelezaji wa Mkataba wa Mfumo itafanyika mnamo tarehe 14 Januari 2025, kisha kutakuwa na hattua ya mwisho ambayo ni mkutano na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa na Ukuzaji wa Ushirikiano wa Umma na Binafsi, Denis Christel. Sassou N'Guesso.