Papa kwa Caritas ya Amerika ya Kusini na Carribien:Muwe kama Malaika kwa wale wanaoteseka na dhuluma
Pope
Kulinda ni neno muhimu ambalo Papa alionesha kwa kazi ya Caritas ya Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribien, ambapo wakurugenzi na marais walikutana siku hizi jijini Roma kwa kozi ya Pili ya mafunzo juu ya “Ulinzi wa watoto.” Baba Mtakatifu Francisko alikutana nao tarehe 15 Januari 2025, katika ukumbi mdogo wa Paul VI kabla ya Katekesi yake na mara moja katika hotuba yake alisisitiza juu ya mwaliko wa "utamaduni wa utunzaji" ambao unaweza kufupishwa kwa neno moja la Ulinzi.
Pamoja na wale wanaougua na kulia kwa ajili ya udhalimu wanaoteseka
Neno ambalo kamusi ya Chuo cha Kifalme cha Lugha ya Kihispania kinalifafanua kuwa "utunzaji, ulinzi, na utetezi”. Lakini kuna maana nyingine ambayo imevutia umakini wa Papa sana kwamba “Ishara ambayo wakati wa vita, kwa amri ya makamanda wa kijeshi, huwekwa kwenye milango ya nchi au kwenye milango ya nyumba ili askari wao wasiharibu." Kwa upande wa Baba Mtakatikfu Francisko, ufafanuzi huu unakumbusha maandishi ya nabii Ezekieli na Ufunuo ambapo tunasoma kwamba: “Bwana alimwambia Malaika wake; weka alama ya Tau kwenye vipaji vya nyuso za watu wanaopumua na kulia kwa ajili ya machukizo yote yanayofanywa humo. Baba Mtakatifu Francisko alisisitiza, “hapa Bwana anatuomba sisi, tuwe wajumbe wake, malaika wake kwa maana ya utume, ingawa si usafi, tuweke alama ya msalaba wake uliobarikiwa katika vipaji vya nyuso za wale wote wanaokuja Caritas yetu, wakiwa na maumivu na wakilia kwa ajili ya dhuluma nyingi, hata machukizo, wanayotendewa.
Wabeba upendo wa Mungu
Kwa hiyo himizo la Papa ni "'karibu' kwa kuweka ishara hii kwa kila mgonjwa, kwa kila mtaalamu, kwa kila mwanadamu tunayekutana naye"; hii, alisema, ni kutambua ndani yake hadhi yake kama ndugu katika Kristo, aliyekombolewa kwa damu ya Mwokozi, ni kuona ndani yake jeraha lililo wazi la Mkombozi ambaye anatupa mkono wake ulionyoshwa ili tutambue fumbo la mwili wake”. Kwa maana hii, ulinzi ni "neno la kimungu, ni Kristo mwenyewe aliyeandikwa kwenye paji la uso la kila mwanamume na kila mwanamke na, kama kwenye kioo, katika moyo wetu ambao, kwa udhaifu wetu, tunataka kuwa wabebaji upendo wake, kwa ishara ndogo za upendo na utunzaji," alisema Papa Francisko.