蜜桃交友

Tafuta

2025.01.15 Papa Francisko alikutana na Marais na wakurugenzi wa kitaifa wa Caritas Baraani Amerika Kusini na Carribien. 2025.01.15 Papa Francisko alikutana na Marais na wakurugenzi wa kitaifa wa Caritas Baraani Amerika Kusini na Carribien.   (Vatican Media)

Papa kwa Caritas ya Amerika ya Kusini na Carribien:Muwe kama Malaika kwa wale wanaoteseka na dhuluma

Papa Fransisko alikutana na wakurugenzi na marais wa mashirika mbalimbali ya Caritas katoliki yaliyoenea katika bara la Amerika ya Kusini ya na kuwahimiza kulinda ikiwa na maana ya utunzaji na kwamba wapeleke upendo wa Kristo kwa ishara ndogo za utunzaji na upendo.

Pope

Kulinda ni neno muhimu ambalo Papa alionesha kwa kazi ya Caritas ya Amerika ya Kusini na Visiwa vya Carribien, ambapo wakurugenzi na marais walikutana siku hizi jijini Roma kwa kozi ya Pili ya mafunzo juu ya “Ulinzi wa watoto.” Baba Mtakatifu  Francisko  alikutana nao tarehe  15 Januari 2025, katika ukumbi mdogo wa Paul VI  kabla ya Katekesi yake na mara moja katika hotuba yake alisisitiza juu ya mwaliko wa "utamaduni wa utunzaji" ambao unaweza kufupishwa kwa neno moja la Ulinzi.

Marais na wakurugeniz wa caritas kitaifa huko Amerika Kusini
Marais na wakurugeniz wa caritas kitaifa huko Amerika Kusini

Pamoja na wale wanaougua na kulia kwa ajili ya udhalimu wanaoteseka

Neno ambalo kamusi ya Chuo cha Kifalme cha Lugha ya Kihispania kinalifafanua kuwa "utunzaji, ulinzi, na utetezi”. Lakini kuna maana nyingine ambayo imevutia umakini wa Papa sana kwamba “Ishara ambayo  wakati wa vita, kwa amri ya makamanda wa kijeshi, huwekwa kwenye milango ya nchi au kwenye milango ya nyumba ili askari wao wasiharibu." Kwa upande wa Baba Mtakatikfu Francisko, ufafanuzi huu unakumbusha maandishi ya nabii Ezekieli na Ufunuo ambapo tunasoma kwamba: “Bwana alimwambia Malaika wake; weka alama ya Tau kwenye vipaji vya nyuso za watu wanaopumua  na kulia kwa ajili ya machukizo yote yanayofanywa humo. Baba Mtakatifu Francisko alisisitiza, “hapa Bwana anatuomba sisi,  tuwe wajumbe wake, malaika wake kwa maana ya utume, ingawa si usafi, tuweke alama ya msalaba wake uliobarikiwa katika vipaji vya nyuso za wale wote wanaokuja Caritas yetu, wakiwa na maumivu na wakilia kwa ajili ya dhuluma nyingi, hata machukizo, wanayotendewa.

Papa alikutana na marais na wakurugenzi kitaifa wa Caritas Amerika Kusini
Papa alikutana na marais na wakurugenzi kitaifa wa Caritas Amerika Kusini

Wabeba upendo wa Mungu

Kwa hiyo himizo la Papa ni "'karibu' kwa kuweka ishara hii kwa kila mgonjwa, kwa kila mtaalamu, kwa kila mwanadamu tunayekutana naye"; hii, alisema, ni kutambua ndani yake hadhi yake kama ndugu katika Kristo, aliyekombolewa kwa damu ya Mwokozi, ni kuona ndani yake jeraha lililo wazi la Mkombozi ambaye anatupa mkono wake ulionyoshwa ili tutambue fumbo la mwili wake”. Kwa maana hii, ulinzi ni "neno la kimungu,  ni Kristo mwenyewe aliyeandikwa kwenye paji la uso la kila mwanamume na kila mwanamke na, kama kwenye kioo, katika moyo wetu ambao, kwa udhaifu wetu, tunataka kuwa wabebaji upendo wake, kwa ishara ndogo za upendo na utunzaji," alisema Papa Francisko.

Papa alikutana marais na wakurugenzi Caritas barani Amerika Kusini
16 January 2025, 12:21