Papa Francisko:Watoto wakue katika imani,ubinadamu wa kweli katika furaha ya familia
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Siku ambayo mama Kanisa anaadhimisha Siku kuu ya Ubatizo wa Bwana Dominika tarehe 12 Januari 2025, amewabatiza watoto 21 wa wafanyakazi wa Vatican katika mazingira ya Kikanisa kizuri sana cha Sistine mjini Vatican. Kwa njia hiyo vilio, kelele, mayowe, na machozi ndizo sauti za kwanza za uwepo, na za asili na za hiari, zilizosikika na kujirudia kati ya picha na kazi za sanaa zinazowakilisha kilele cha zawadi na talanta zilizotolewa kwa ubinadamu katika maisha yote.
Zawadi kuu zaidi: imani
Kabla ya Maadhimisho hayo Baba Mtakatifu Francisko alishirikisha mapendekezo yake ya kawaida, yenye kufikiria kwamba: "Ni muhimu watoto wajisikie vizuri!" Sofia, Vittoria, Tancredi Tito, Edwin Gabriele na watoto wengine 17, na kwamba "leo wanaongoza na lazima tuwahudumie, kwa Sakramenti, na kwa sala." Papa aliongeza kusema " Akina mama ninaalikwa kama kawaida kunyonyesha watoto wenu ikiwa wana njaa na kuwabadilisha ikiwa wana joto. Leo kila mmoja wenu wa wazazi na Kanisa lenyewe, linatoa zawadi kuu zaidi, ambayo ni zawadi ya imani kwa watoto.” Papa Francisko alisema.
Ishara ya msalaba kwenye paji la uso la watoto wadogo
Huku mikono ikitetemeka kwa hisia, wazazi walimwendea Mrithi wa Petro ili watoto wao wapokee ishara ya msalaba kwenye vipaji vya nyuso zao. Wengine walipiga teke, lakini wengine walitulia kwa sababu walikuwa wamelala au bado ni wadogo sana. Papa Fransisko aliwakaribisha kila mtu kwa tabasamu na, ikiwa kuna kaka au dada mdogo, aliwaruhusu watie alama ya msalaba kwenye mapaja ya nyuso za wale watakaobatizwa. Sherehe ilipamba moto, sauti za Schola Cantorum kwa wimbo kwa ajili ya watoto wadogo, ukiwalegeza baadhi yao kwenye usingizi wa amani. Kwa hakika, kulikuwa na vilio vichache vinavyounda liturujia ya Neno. Kwa mujibu wa mapokeo, ni maneno yaliyotamkwa na Papa katika mahubiri yake - ili "kutowachosha" watoto wadogo, aliyokuwa amesema katika sherehe zilizopita. "Wakue katika imani",Papa Francisko anatumaini, kwamba watoto waweze kuonja ubinadamu wa kweli, katika furaha ya familia.
Liturujia iliendelea na wakonselebranti, ambapo Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo na Kardinali Fernando Vérgez Alzaga, Rais wa Mji wa Vatican waliwaweka kifuani kwa kila anayebatiza mafuta ya katekumeni. Kisha, Papa Francisko alitoa Sakramenti ya Kikristo, huku akiwalowesha kichwa cha kila mtoto kwa maji matakatifu, wakiwa wamesindikizwa na wazazi, pia wazazi wa ubatizo(godfathers and godmothers). Na kisha upako wa mafuta ya chrisma. Kardinali Krajewski aliendeleza na ishara ya kuweka mikono yao juu ya kila mtu aliyebatizwa kwa kubembeleza.
Wakati Kardinali Vérgez Alzaga ndiye aliyetoa vazi jeupe, huku kila baba mzazi akiwa na kazi ya kupeleka na kuwasha mshumaa wake kutoka katika mwali mkuu wa mshumaa wa Pasaka. Hii ni kubeba nuru hii iwe, katika nyumbani watoto kama ukumbusho wa siku hiyo. Na inapotokea shida au shida yoyote, wawashe taa ili kumwomba Bwana Neema, kwa ajili ya familia yao. Ibada ya "Effatà", ya "funguliwe", pia ili fanywa, ambayo inachukuliwa katika sehemu ya Injili ya Marko ambapo Yesu alimponya kiziwi-bubu. Makardinali wawili waligusa masikio na midomo ya watoto waliobatizwa kwa vidole gumba.
Mwishoni mwa maadhimisho Papa Francisko alitumia fursa hiyo kusalimia familia za waliobatizwa na kubadilishana maneno machache huku akitoa zawadi kwa kila mmoja wao. Utoaji wa Ubatizo kwa watoto wa wafanyakazi wa Vatikani ni sehemu yya utamaduni ulioanzishwa mnamo 1981 na Mtakatifu Yohane Paulo II na marekebisho moja tu: kwa miaka miwili ya kwanza ubatizo ulifanyika katika Kikanisa cha Pauline, lakini kuanzia 1983 hadi sasa ni katika Kikanisa cha Sistine jijini Vatican.