Papa Francisko asaidia familia kubwa na kuwapa msaada wa kifedha
Pope
Kuanzia tarehe 1 Januari 2025, familia zilizo na watoto kuanzia watatu au zaidi zitapokea ('bonusi') bonasi ya kila mwezi ya euro 300.00. Hivi ndivyo Baba Mtakatifu Francisko aliamua kwa wafanyakazi wa kudumu wa mji wa Vatican. Kiasi hicho kufuatia na taarifa kwa vyombo vya habari inasema kuwa inatolewa hadi umri wa miaka 18 au hadi mwisho wa mzunguko wa kawaida wa masomo, la muhimu imeandikwa na cheti cha uandikishaji kilichotolewa na shule ya sekondari au chuo kikuu, na kwa hali yoyote si zaidi ya umri wa miaka 24.
Zaidi ya hayo, barua hiyo inaeleza kuwa Papa amethibitisha kwamba likizo ya wazazi itaongezeka kutoka siku tatu hadi siku tano za sasa. Kiukweli, siku tatu za likizo za kulipwa wakati mtoto anapozaliwa, pia zinatumika kwa baba wa kuasili au mlezi, zinaongezwa hadi tano. Huu ni mpango binafsi wa Baba Mtakatifu, uliowasilishwa na Papa mwenyewe kwa Kardinali Fernando Vérgez Alzaga na kwa Sr. Raffaella Petrini, ambao ni rais na katibu mkuu wa mji wa Vatican, wakati wa mkutano uliofanyika Alhamisi ya tarehe 19 Desemba 2024, pamoja na maagizo ya kuendelea mara moja.