Papa alitembelea Mfuko wa Roma wa mipango inayowasilishwa katika Maeneo ya Vita na Umaskini
Na Salvatore Cernuzio na Angella Rwezaula – Vatican.
Chini ya nusu saa katika makao makuu ya Shirika la Mfuko wa Roma, ndani ya Jengo la Sciarra Colonna la kihistoria, linalotazama njia ya Corso hatua chache kutoka Jumba la kumbukumbu ambapo, mnamo tarehe 8 Desemba 2024 alikuwa amekwenda kustaajabia maonesho ya Chagall ya Msalaba Mweupe. Tukio lingine la mshangao alasiri tarehe 11 Januari 2025, Papa Francisko alikwenda kwenye makao makuu ya kile ambacho mnamo 1500 kilizaliwa kama Monte di Pietà ya Roma na Barua ya Papa Paulo III, na ambapo leo hii ni shirika linalofanya kazi katika sekta tano za kuingilia kati shida, ili pasiwe anayebaki nyuma kwa njia ya Shirika la Mfuko wa Roma. Ni Mfuko wa kihistoria kwa sababu ulianza karne ya 17 na kujulikana kama Kanisa la Chagall. Mfuko huo unajikita na shughuli za afya, utafiti wa kisayansi, usaidizi wa aina zisizojiweza kijamii, elimu katika mafunzo, utamaduni, jumuiya ya ustawishaji inayongozwa katika kanuni za mshikamano katika usaidizi.
Asante kwa kujitolea na ukarimu
Rais wa Shirika la Mfuko wa Roma Franco Parasassi alimkaribisha Papa, ambaye alifika kwa gari, kwenye mlango wa jengo la kale. Pamoja naye, wajumbe wa Kamati ya Uongozi, Bodi ya Wakurugenzi, Bodi ya Wakaguzi wa Hesabu na mkurugenzi mkuu Renato Lattante. Baadhi ya wanafamilia pia walikuwepo. Salamu na kubadilishana maneno mawili, matatu na kisha Papa Francis alikwenda kwenye Kikanisa kidogo kilichojengwa ndani ya Jengo hilo na kukibariki. Katika Ukumbi wa Mikutano Papa alizungumza na viongozi wa Mfuko huo na aliwashukuru kwa "dhamira iliyooneshwa katika shughuli zake za kitaasisi, na umuhimu wa kujitoa bure katika maeneo yote na hasa, katika tamaduni." Taarifa kupitia msemaji mkuu wa Vyombo vya habari Vatican alibainisha kuwa Papa pia alitoa wito wa kawaida wa kutopoteza ucheshi ulikuwa mwaliko ambao umekuwa ukielekezwa kwa kila mtu, wawe mapadre, wanasiasa hadi watu wa kawaida. Ucheshi ambao ni lazima uambatane na maisha ya kila siku ya kila mtu, Papa Francisko alisisisitiza huku akikumbuka pia sala ya Mtakatifu Thomas More ambayo, kama alivyoweka wazi siku zilizopita kwamba, anasali kila siku
Kumbukumbu ya ziara ya 2019 kwenye "Alzheimer Village"
Kwa upande wake, Rais Parasassi alimshukuru Papa kwa niaba ya Mfuko huo kwa ziara hiyo ya kipekee kabisa, na akakumbuka ziara nyingine mbili: za hivi karibuni ambapo tayari imetajwa huko Jumba la Cipolla, katika eneo la Makumbusho ya Njia ya Corso - kitovu cha Makumbusho, kwa Msalaba Mweupe" na Chagall, kazi iliyopendwa sana na iliyohifadhiwa katika nakala katika utafiti wa Papa, na ziara ya mnamo Aprili 2019 katika "Kijiji cha Alzheimer" eneo la Bufalotta la mji mkuu, Roma, kituo kilichowekwa kwa utunzaji wa watu walioathiriwa na ugonjwa huo ambapo Papa Francisko alikuwa amekwenda kama sehemu ya "Ijumaa ya Huruma." Alasiri hiyo Papa alifika kwa mshangao katika "Kijiji" hicho kuwatembelea wazee walioathiriwa na Alzheimer's lakini pia na Parkinson, wakati huo wakipumzika katika vyumba vyao au kushiriki katika shughuli za burudani, na alikuwa amesisitiza ukaribu wake kwa watu ambao, hata kutokana na ugonjwa wao, wanahatarisha upweke na kutengwa. Matukio na maneno yaliyokumbukwa alasiri hiyo kwamba: "Alzheimer Village" kiukweli inasimamiwa na Mfuko wa Roma ambao unatoa mfano wa mbinu ya utunzaji kwa Italia.
Mipango ya kibinadamu ulimwenguni
Hata hivyo Mfuko huo unaelemewa na majukumu mengi leo hii, Parasassi alimweleza Papa: "Kila mtu anatutazama ili kukidhi mahitaji yanayozidi kuwa magumu na yanayoenea." Katika hali ya dharura, shirika hujibu kwa kupanua shughuli zake nje ya nchi na mipango ya kibinadamu na afya. Kwa hakika, Papa Francisko alikabidhiwa mipango iliyofanywa huko Argentina,huko Bahia Blanca, jimbo la Buenos Aires, kusaidia watu waliokumbwa na dhoruba mbaya mwezi Desemba mwaka 2024; kisha mipango ya Togo, katika Jimbo Kuu la Lomé, kuipatia jamii ya eneo hilo vifaa vya ultrasound kwa ajili ya wanawake wajawazito; tena, katika wilaya ya Bethlehemu kwa ajili ya kuimarisha huduma za kijamii na afya, katika Lebanon na katika Ukraine kwa manufaa ya watu wanaoteswa na vita. Juhudi zote zinazofanywa kupitia vyombo vilivyounganishwa na Kanisa ambavyo huongezwa kwa maingiliano ya kiutamaduni yanayofanywa na Caritas na Jimbo la Roma (ambayo ya mwisho ilipendelea parokia za nje kidogo), na Chama cha Mtakatifu Pietro.