Juma la maombi kwa ajili ya Umoja wa Wakristo,Masifu ya Papa na Kumbukizi ya Baraza la Nikea
Pope
Miaka 1,700 imepita kwani ilikuwa 325 AD. C. tangu wakati ule lilipofanyika Baraza la kwanza la kiekumene la kihistoria, huko Nikea, eneo linaloitwa Uturuki leo hii. Katika tukio la maadhimisho hayo, kwa hiyo Juma la Kuombea Umoja wa Wakristo, ambalo itaadhimishwa kuanzia tarehe 18 hadi 25 Januari 2025, likiwa na maana maalum. Katika tarehe hiyo ya mwisho, maadhimisho ya Uongofu wa Mtakatifu Paulo tarehe 25 Januari, saa 11:30 jioni, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Nje ya Kuta, Baba Mtakatifu Francisko ataadhimisha Masifu ya Jioni.
Mkesha wa kutembea
Kwa siku ya Alhamisi tarehe 23 Januari saa kumi na mbili jioni, Jimbo la Roma imeandaa mkesha wa kutembea katika maadhimisho ya Jubilei inayotualika kuwa “mahujaji wa matumaini” ambapo mkesho huo utahusisha maeneo matatu tofauti ya ibada: Kanisa la Kilutheri kupitia njia ya Sicilia, Kanisa la Kiorthodoksi la Mtakatifu Andrea, kupitia njia ya Sardegna, na parokia ya Mtakatifu Camillo wa Lellis, kupitia Njia ya Piemonte. Kwa hivyo, si mkesha rahisi wa maombi, bali ni hija fupi katika hatua tatu, yenye tafakari tatu za kibiblia zitakazotolewa na Mchungaji Mirella Manocchio kwa ajili ya Wainjili na Mchungaji Simeone Katzinas kwa Kanisa la Kiorthodox na Kanisa Katoliki na Askofu Paolo Ricciardi, mjumbe wa jimbo kwa ajili ya uekumene na majadiliano. Katika kila Kanisa, zitawashwa taa na tafakari zitatolewa, zikiashiria mwanga na matumaini.
Mada ya Juma la Maombi: "Je, unaamini hili?" ( Yh 11, 26 )
"Utoaji huu wa zawadi pia unawakilisha mzunguko, ushirikiano na utofauti katika imani moja", alisisitiza Monsinyo Marco Gnavi, mkuu wa Ofisi ya Uekumene na Majadiliano ya Kidini ya Jimbo la Roma ambapo Kauli mbiu inayoongoza Juma hili ni “Je, unaamini hili?” Kutoka Injili ya Yohane 11, 26. Sala na tafakari hizo ziliandikwa na kaka na dada wa Jumuiya ya Kimonaki ya Bose, kaskazini mwa Italia; timu ya kimataifa iliyoteuliwa na Baraza la Kipapa kwa ajili ya Kukuza Umoja wa Wakristo na Tume ya Imani na Utaratibu ya Baraza la Makanisa Ulimwenguni ilifanya kazi pamoja na watayarishaji. Mada hiyo inapata msukumo kutoka katika mazungumzo kati ya Yesu na Martha, wakati wa ziara ya Yesu kwenye nyumba ya Martha na Maria huko Bethania, baada ya kifo cha ndugu yao Lazaro, kama ilivyosimuliwa na mwinjili Yohane.
Kukumbuka Baraza la Nikea
Monsinyo Gnavi aliendelea kusema: “Mada iliyochaguliwa kwa mwaka huu imechukuliwa kutoka katika mazungumzo kati ya Yesu na Martha katika kukabiliana na changamoto ya kifo cha Lazaro na imani ya Ufufuko katika Kristo. Mada kuu, kwa sababu leo ​​si Makanisa pekee, bali pia watu wanapaswa kukumbana na maneno mengi ya kifo cha kweli, ambacho kinamaanisha pia mgawanyiko, utengano, hadi migogoro na mauaji ya watu wasio na hatia. Hata katika maisha ya kibinafsi ya kila mtu - anaendelea kuhani -, wengi wako peke yao na kutokuwa na uhakika wa sasa kunaleta hitaji la majibu. Mazungumzo kati ya Yesu na Martha yanaonesha jinsi gani katika kila mwanamume na kila mwanamke kuna swali la imani lililo wazi au la wazi. Maneno haya pia yanatusaidia kukumbuka ukumbusho wa Mtaguso wa Nikea, ambao ulitupatia kukiri sala yaNasadiki na imani inayotuunganisha sisi sote katika Ubatizo.”