ҽ

Kardinali  Wilton Daniel Gregory Askofu Mkuu wa  Washington, nchini Marekani. Kardinali Wilton Daniel Gregory Askofu Mkuu wa Washington, nchini Marekani. 

Washington,Kard.D.Gregory:kama watu wa imani na nia njema,tumeitwa kutafuta ukweli

Kufuatia uchaguzi wa Rais mpya wa Marekani,Kardinali Daniel Gregory,Askofu Mkuu wa Washington alitoa maoni yake tarehe 6 Novemba 2024:”Baadhi ya watu leo wanapumua kutokana na matokeo ya uchaguzi wetu wa kitaifa,majimbo na mitaa,hata kama wengine wanakabiliwa na wasiwasi kuhusu wakati wetu ujao.Njia yetu ya kusonga mbele iko katika heshima yetu sisi kwa sisi na hadhi tuliyopewa na Mungu tunayoshiriki,inayotolewa bure kwa sala,subira,fadhili na tumaini.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kardinali Wilton Gregory, Askofu Mkuu wa Washington, alitoa taarifa ifuatayo  tarehe 6 Novemba 2024  kufuatia uchaguzi mkuu wa 2024 uliofanyika kwamba “Leo, wakati taifa letu linapojiandaa kuchukua mwelekeo mpya katika utawala, ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu kukumbuka kwamba, kama watu wa imani na nia njema, tumeitwa kufanya kazi pamoja kutafuta ukweli, haki na amani katika nchi yetu, nyumbani, katika jamii zetu, na katika taifa letu.”

Mungu ibariki Nchi ya Marekani

Askofu Mkuu wa Jiji la Washingtoa aidha aliongeza: “Baadhi ya watu leo ​​wanapumua kwa utulivu kutokana na matokeo ya uchaguzi wetu wa kitaifa, majimbo na mitaa, hata kama wengine wanakabiliwa na wasiwasi kuhusu maisha yetu ya baadaye. Njia yetu ya kusonga mbele iko katika heshima yetu kuheshimiana sisi kwa sisi na katika hadhi tuliyopewa na Mungu tunayoshiriki, ambayo inayotolewa bure kwa sala, subira, fadhili na tumaini.” Kwa kuhitimisha Kardinali Gregory alisema: “Mungu ibariki Nchi ya Marekani.”

Maneno ya kwanza  ya Trump

Rais wa zamani Donald Trump alichaguliwa kwa muhula wa pili katika Ofisi ya Oval miaka minne baada ya kupoteza muhula wake wa pili mfululizo, kulingana na makadirio mengi. Uchaguzi wa Trump uliofanyika Novemba 5 unaashiria hitimisho la msimu wa kampeni wenye misukosuko uliojumuisha hata majaribio mawili ya kumuua. “Nataka kuwashukuru watu wa Marekani kwa heshima kubwa ya kuchaguliwa kuwa rais wenu wa 47 na rais wenu  wa 45,” Trump aliwaambia wafuasi wake huko West Palm Beach, Florida, mwendo wa saa 8:30 asubuhi ya  Novemba 6, na kuongeza, “Hii itakuwa kweli enzi ya dhahabu ya Amerika.”

Maoni ya Kardinali Gregory wa Washington-Marekani
07 November 2024, 09:54