Vipaumbele vya 2025 vya Rais wa Baraza Kuu la UN
Kutoka Umoja wa Mataifa
Bwana Philémon Yang, Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) tarehe 14 Januari 2025 aliorodhesha maeneo makuu ya shughuli na matukio ya ngazi ya juu kwa mwaka huu wa 2025 akisema kuwa lugha mbalimbali na uwezeshaji wa wanawake itakuwa ni masuala mtambuka yatakayopewa uzito na kiongozi wa chombo hicho cha kujadili, changamoto zinazoikabili dunia ambazo zinahitaji kujitolea kufanya kazi pamoja. Bwana Yang, alitoa wito wa azimio la pamoja kutoka kwa nchi wanachama kushughulikia changamoto kubwa zaidi za kimataifa. Aliwasilisha vipaumbele vya kikao cha 79 cha baraza hilo, kinachoendelea hadi Septemba mwaka huu.
Vipaumbele vya 2025
Mambo muhimu ni pamoja na ufadhili wa maendeleo, kutokomeza ajira kwa watoto na kufikia amani na usalama barani Afrika. Ametaja mada nyingine zitakazopewa kipaumbele kuwa ni kupambana na utumiaji haramu wa silaha ndogo ndogo na nyepesi, kulinda utu wa binadamu katika migogoro ya kivita, na kuharakisha Malengo ya Maendeleo Endelevu, ikiwa ni pamoja na kupitia mfumo wa kidijitali. Yang alisema lugha mbalimbali na uwezeshaji wa wanawake itakuwa masuala mtambuka katika kiini cha vipaumbele hivi. Mipango hiyo inalenga kuhuisha kazi ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Likiwa na wanachama wake nchi 193, ni chombo hicho kinawakilisha jukwaa pana zaidi la majadiliano ya kimataifa.
Kuzingatia utekelezaji wa Mkataba wa Zama jijazo
Rais huyo wa Baraza Kuu alisema changamoto zinazoikabili dunia zinahitaji kujitolea na kufanya kazi pamoja ili kufikia malengo ya pamoja. Yang pia aliakisi mfumo unaowakilishwa na Mkataba wa Zama Zijazo na viambatanisho vyake, Mkataba wa Kimataifa wa Kidijitali na Azimio la Vizazi Vijavyo, liliyopitishwa Septemba 2024. Kwake Yeye makubaliano haya yaliweka misingi ya mfumo mpya wa kimataifa uliokubaliwa na hali halisi ya ulimwengu wa leo na changamoto za kesho. Rais wa Baraza Kuu alisema ataunga mkono nchi wanachama katika kutekeleza Mkataba huo kwa kuandaa midahalo mitatu isiyo rasmi. Mikutano hii itatoa fursa kwa majadiliano ya wazi, jumuishi na yenye mwelekeo wa kuchukua hatua, kwa lengo la kupanga njia ya kusonga mbele.
Kukusanya rasilimali kwa ajili ya amani
Yang alisema kuwa urais wake “utajengwa juu ya kanuni za umoja katika utofauti, na kukuza mazingira ambapo kila sauti sio tu inasikika, bali inathaminiwa." Kiongozi huyo wa Baraza Kuu alisema mwaka 2025 unaanza huku zaidi ya watu bilioni 1 wakiwa bado wanaishi katika umaskini uliokithiri, na asilimia 40 kati yao wakiwa katika nchi zilizokumbwa na migogoro mikubwa. Alitoa mfano wa Gaza, Sudan na Ukraine, ambapo migogoro "inaua maelfu ya watu, kufurusha mamilioni ya watu na kusambaratisha nchi hizo." Pamoja na matumizi ya kijeshi kuongezeka kwa kasi, rais huyo amesisitiza kwamba "vita sio na kamwe haitakuwa chaguo endelevu la kutatua migogoro na majanga." Alitoa wito wa kuhamasishwa kwa rasilimali za kifedha, kisayansi na kisiasa, "si kwa silaha za vifo na uharibifu, bali kwa maendeleo, amani na ustawi."
Matukio makuu ya ngazi ya juu
Kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kitaandaa mijadala kadhaa ya ngazi ya juu mwaka 2025, ikiwa ni pamoja na:
? Mkutano wa ngazi ya juu wa kuadhimisha kumbukumbu ya miaka thelathini ya Mpango wa Utekelezaji wa Vijana Duniani.
? Mkutano wa kimataifa wa Kijamii na Maendeleo
? Mkutano wa ngazi ya juu wa kusherehekea kumbukumbu ya miaka 30 ya Mkutano wa 4 wa Dunia wa Wanawake
? Mkutano wa 4 wa Kimataifa wa Ufadhili wa Maendeleo
? Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu vikwazo vya kimuundo vinavyokabili nchi za kipato cha kati katika kutekeleza Ajenda ya 2030.
? Majadiliano ya Ngazi ya Juu kuhusu Utamaduni na Maendeleo Endelevu
? Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Dhoruba ya Mchanga na Vumbi
? Mkutano wa Kilele wa Dunia wa Jumuiya ya Habari
? Kuundwa kwa Jopo Huru la Kimataifa la Kisayansi kuhusu Akili Mnemba (AI)
? Mkutano wa 3 wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya Bahari
? Matukio ya Muongo wa Pili wa Kimataifa kwa Watu Wenye Asili ya Kiafrika
? Mkutano wa ngazi ya juu wa kuadhimisha miaka 25 ya Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake.