蜜桃交友

Tafuta

mazishi ya wale waliokufa katika Shambulizi la kigaidi huko Ankara dhidi ya makao makuu ya tasnia ya anga nchini Uturuki. mazishi ya wale waliokufa katika Shambulizi la kigaidi huko Ankara dhidi ya makao makuu ya tasnia ya anga nchini Uturuki.  (AFP or licensors)

Mashambulizi huko Ankara dhidi ya makao makuu ya tasnia ya anga nchini Uturuki

Wanne wamefariki na 14 kujeruhiwa,3 kati yao wako hali mbaya.Haya ni matokeo ya shambulio la kigaidi lililotokea alasiri Oktoba 23 dhidi ya makao makuu ya tasnia ya anga nchini Uturuki ambao ni muundo wa ulinzi wa Uturuki,yapata kilomita arobaini kutoka Ankara.

Na Stefano Leszczynski na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika shambulizi la kigaidi dhidi ya makao makuu ya tasnia ya anga nchini Uturuki yaliyotokea alasiri tarehe 23 Oktoba 2024 yalisababisha karibia vifo 4 na watu 14 kujeruhiwa. Kutoka NATO mshikamao kwa Rais wa Jamhuri hiyo, Bwana Erdogan na kwa nchi nzima. Hata hivyo Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye yuko nchini Urusi kwa ajili ya  mkutano wa kilele wa nchi za Kbarkani huko Kazan, mara moja alipokea mshikamano kutoka kwa Rais Putin wa Urusi, ambaye aliwasilisha salamu zake za rambirambi hata kwa nchi hiyo.

Shambulio hilo

Shambulio hilo ambalo bado halijadaiwa, lilianza saa kumi jioni kwa saa za huko na lilidumu kwa takriban saa moja na nusu, kama inavyothibitishwa na video kutoka katika kitengo cha uchunguzi wa ndani ambacho kilirekodi awamu zote za shambulio hilo. Kwa mujibu wa taarifa za awali zilizotolewa na vyombo vya habari nchini humo, ni shambulio la kujitoa mhanga huku mmoja wa washambuliaji akijilipua kwenye mlango wa jengo hilo na wengine wawili kuuawa wakati wa operesheni hiyo..

Athari za kimataifa

Mwitikio wa Katibu Mkuu wa NATO Mark Rütte ulikuwa wa haraka, akitangaza ukaribu na mshikamano na Uturuki, mwanachama wa Muungano huo. Rambirambi na ukaribu kwa nchi pia zilioneshwa na uwakilishi wa Umoja wa Ulaya huko Ankara na na serikali za kibinafsi za Muungano wa Atlantic.

Maoni ya Uturuki

Wizara ya sheria ya Uturuki imefungua uchunguzi wa kuchunguza tukio hilo. "Haturudisha hatua kamwe  nyumba kutoka katika tasnia ya ulinzi na njia ya mpango wa kiteknolojia wa kitaifa. Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Teknolojia Mehmet Fatih Kachir, akitoa maoni yake juu ya shambulio la kigaidi kwenye kampasi ya Kahramankazan ya tasnia ya anga ya Uturuki. Tai – alikumbusha katika Kituo cha (CNN Turk )- kuwa hivi majuzi kimetengeneza helikopta nyingi, magari ya anga na ndege zisizo na rubani kama vile Anka na Aksungur, helikopta ya shambulio la Atak, Gökbey, Hürku?, Hürjet na helikopta za madhumuni ya jumla ya Kaan.

Mafundi wa Leonardo wako salama

Pia kulikuwepo na mafundi 8 wa Uwanja wa Ndege wa Leonardo da Vinci (Italia) katika eneo la kiwanda, hicho ambao  mara moja  walimjulisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Italia Bwana Tajani, " kuwa wako vizuri na salama."

Mashambulizi mengine ya awali

Tayari mnamo Januari, Istanbul ilikuwa eneo la shambulio lililodaiwa na waliojiita Islamic State- Serikali ya Kiislamu dhidi ya Kanisa ambalo lilisababisha kifo cha mtu mmoja. Mnamo Oktoba 2023, shambulio lilitekelezwa dhidi ya kituo cha polisi na seli ya PKK. Shambulio la Jumatano 23 Oktoba  limefanyika sambamba na ufunguzi wa maonesho ya makampuni ya anga mjini Istanbul.

Shambulio la kituo cha Utafiti wa Anga huko Ancara nchini Uturuki
24 October 2024, 12:07