Akili Mnemba yaunda njia mpya ya kufikiri,mafunzo juu ya Tabia ya asili ya mwanadamu!
Pope
Mwingiliano kati ya binadamu na Akili Mnemba(IA)unatoa sura kwa mfumo mpya wa fikra, mpango mpya wa utambuzi ulio nje ya akili ya mwanadamu lakini wenye uwezo wa kuongeza uwezo wake wa utambuzi, unaoitwa ‘Mfumo 0’, ambao umewekwa kando ya mifano miwili ya mawazo ya binadamu ambayo huifanya Mfumo wa 1, wenye sifa ya kufikiri angavu, wa haraka na automatiki, na Mfumo wa 2, wazo moja la uchanganuzi zaidi na tafakari. Hata hivyo, Mfumo 0 unaanzisha kiwango zaidi cha utata, ukibadilisha kwa kiasi kikubwa mazingira ya utambuzi ambamo tunafanyia kazi na kwa hivyo inaweza kuashiria hatua ya milele katika mageuzi ya uwezo wetu wa kufikiri na kufanya maamuzi. Itakuwa jukumu la ubinadamu kuhakikisha kuwa maendeleo haya yanatumiwa kwa njia ambayo inaboresha uhuru wetu wa utambuzi, bila kuathiri.
Kesi za tabia ya asili ya binadamu
Haya ndiyo yaliyoripotiwa katika jarida maarufu la kisayansi la Nature Human Behavior yaani Tabia asili za Binadamu ambalo lilichapisha makala yenye kichwa: yaani “Kesi ya mwingiliano wa binadamu na Akili Mnemba (AI) kama mfumo wa kufikiri wa Mfumo 0 iliyoandikwa na timu ya watafiti iliyoratibiwa na Profesa Giuseppe Riva, mkurugenzi wa Humane Technology Lab, yaani ‘Maabara ya Teknolojia ya Binadamu’, wa Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu, kwenye Campasi ya Milano na wa Maabara ya Teknolojia Inayotumika kwa Neuro-Saikolojia katika Taasisi ya Italia ya Auxological IRCCS, Milano. Utafiti huo ulifanywa na Mario Ubiali mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa kuanzisha Thimus, Massimo Chiriatti wa Infrastructure Solutions Group-yaani ‘Kikundi cha Suluhu za Miundombinu’ Lenovo, huko Milano, Profesa Marianna Ganapini wa idara ya Falsafa ya Union College, Schenectady –yaani ‘ Chuo cha Muungano, Schenectady huko New York, Marekani, Profesa Enrico Panai wa Kitivo cha Lugha za Kigeni na Lugha ya Sayansi katika Chuo Kikuu Katoliki cha Moyo Mtakatifu, kwenye kampasi ya Milano.
Aina mpya ya mawazo ya nje
Kama vile diski kuu ya nje hukuruhusu kuhifadhi data ambayo haipo kwenye kompyuta, data ya kufanya kazi kwa kuiunganisha na Kompyuta popote tulipo, vivyo hivyo akili Mnemba (IA), pamoja na uwezo wake wa galaksi wa kuhesabu na usindikaji wa data, inaweza kuwakilisha mzunguko wa nje wa ubongo wa mwanadamu katika uwezo wa kuuimarisha. Kwa hivyo wazo la mfumo 0 ambao sio zaidi ya aina ya fikra za nje kulingana na uwezo wa AI. Kwa kushughulikia idadi kubwa ya data, Akili Mnemba inaweza kuchakata maelezo na kutoa mapendekezo au maamuzi kulingana na algoriti changamano. Walakini, tofauti na fikra angavu au uchanganuzi, Mfumo 0 hauhusishi maana ya ndani kwa habari inayochakata. Kwa maneno mengine, AI inaweza kufanya mahesabu, utabiri, na kutoa majibu bila kuelewa maudhui ya data ambayo inafanya kazi nayo. Kwa hivyo, wanadamu wanabaki kuwa muhimu kutafsiri na kutoa maana kwa matokeo yanayotolewa na Akili Mnemba(AI.) Ni kama kuwa na msaidizi anayekusanya, kuchuja na kupanga maelezo kwa njia ifaavyo, lakini bado kunahitaji kuingilia kati kwetu ili kufanya maamuzi sahihi. Usaidizi huu wa utambuzi hutoa mchango muhimu, lakini udhibiti wa mwisho lazima daima ubaki mikononi mwa mwanadamu.
Hatari za Mfumo 0:kupoteza uhuru na uaminifu kipofu
Kwa mujibu wa maprofesa Riva na Ubiali walisisitiza kuwa: “Hatari ni kutegemea sana Mfumo 0 bila kufikiria kwa kina. Ikiwa tutakubali kwa urahisi masuluhisho yanayotolewa na AI, tunaweza kupoteza uwezo wetu wa kufikiri kwa kujitegemea na kukuza mawazo ya kibunifu. Katika muktadha unaozidi kutawaliwa na uautomatiki, ni muhimu kwamba wanadamu waendelee kuhoji na kujihoji matokeo yanayotokana na Akili Mnemba AI,” wataalam hao walisisitiza. Zaidi ya hayo, “uwazi na uaminifu katika mifumo ya AI inawakilisha tatizo lingine kuu. Tunawezaje kuwa na uhakika kwamba mifumo hii haina upendeleo au upotoshaji, na kwamba hutupatia taarifa sahihi na zinazotegemeka?” “Mwelekeo unaokua wa kutumia data sanisi au iliyochakatwa kihalisi inaweza kuathiri mtazamo wetu wa ukweli na kuathiri vibaya mchakato wetu wa kufanya maamuzi,” wanaonya wataalamu hao AI inaweza hata kuteka uwezo wetu wa kujichunguza, wanataja, kitendo cha kutafakari mawazo na hisia za mtu -ambapo ndiyo mchakato wa kipekee wa kibinadamu. Hata hivyo, kwa maendeleo ya AI, inaweza kuwezekana kutegemea mifumo yenye akili kuchanganua tabia na hali zetu za kiakili. Hii inatuongoza kuuliza: ni kwa kiwango gani tunaweza kujielewa wenyewe kupitia uchambuzi wa AI? Na je, akili ya mnemba inaweza kuiga ugumu wa uzoefu wa kibinafsi?
Fursa kubwa
Hata na maswali haya yote, Mfumo 0 pia hutoa fursa kubwa, wanakumbuka maprofesa. Shukrani kwa uwezo wake wa kuchakata data changamano haraka na kwa ufanisi, AI inaweza kusaidia ubinadamu katika kushughulikia matatizo ambayo ni zaidi ya uwezo wetu wa asili wa utambuzi. Iwe inasuluhisha maswali changamano ya kisayansi, kuchambua hifadhidata kubwa au kudhibiti mifumo tata ya kijamii, AI inaweza kuwa mshirika asiyeweza kubadilishwa. Ili kutumia vyema uwezo wa Mfumo 0, waandishi wa kazi wanapendekeza, ni muhimu kuunda miongozo ya maadili na uwajibikaji kwa matumizi yake. “Uwazi, uwajibikaji na ujuzi wa kidijitali ni vipengele muhimu vya kuruhusu watu kuingiliana kwa umakini na AI,” wanaonya Riva na Ubiali. Kuelimisha idadi ya watu kuhusu jinsi ya kukabili mazingira haya mapya ya utambuzi kutakuwa jambo la msingi ili kuepuka hatari za utegemezi kupita kiasi kwenye mifumo hii.
Mustakabali wa mawazo ya mwanadamu
Ikiwa hautadhibitiwa, Mfumo 0 unaweza kuingilia mawazo ya mwanadamu katika siku zijazo, wanahitimisha: “ni muhimu kwamba tuendelee kufahamu na kukosoa jinsi tunavyoitumia; Uwezo wa kweli wa Mfumo 0 utategemea uwezo wetu wa kuuelekeza katika mwelekeo sahihi.”