蜜桃交友

Tafuta

Kardinali Zuppi Rais wa CEI na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Bologna, Italia. Kardinali Zuppi Rais wa CEI na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Bologna, Italia.  (ANSA)

Ukraine:Simu kati ya Kard.Zuppi na Li Hui kuhusu mazungumzo ya amani

Tarehe 14 Agosti 2024,mazungumzo ya kirafiki yalifanyika kati ya Bwana Li Hui,Mwakilishi Maalum wa Serikali ya China katika Masuala ya Ulaya na Asia, na Kardinali Matteo Zuppi,kama sehemu ya utume uliokabidhiwa kwa Kardinali huyo na Papa Francisko kwa ajili ya amani nchini Ukraine na kufuatia mkutano wa Beijing mnamo Septemba 2023.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kupitia taarifa ya Vyombo vya habari Vatican iliyotolewa tarehe 15 Agosti 2024 imebainisha kuwa: “Asubuhi ya tarehe 14 Agosti 2024, mazungumzo ya kirafiki yalifanyika kati ya Bwana Li Hui, Mwakilishi Maalum wa Serikali ya China katika Masuala ya Ulaya na Asia na Kardinali Matteo Zuppi, Rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI),  kama sehemu ya utume aliokabidhiwa Kardinali huyo na Papa Francisko kwa ajili ya amani nchini Ukraine na kufuatia mkutano wa Beijing  mnamo Septemba iliyopita mwaka 2023.” Kwa njia hiyo: “Wakati wa mazungumzo na simu, taarifa inabainisha kuwa “wasiwasi mkubwa ulioneshwa kwa hali hiyo na haja ya kuhimiza mazungumzo kati ya Vyama, na dhamana ya kutosha ya kimataifa kwa ajili ya amani ya haki na ya kudumu.” Simu hiyo ilifanyika karibu mwaka mmoja baada ya safari ambayo Kardinali Matteo Zuppi alifanya mnamo Septemba 2023 ya kwenda Jijini Beijing.

Kituo cha Nne  Nchini cha Mjumbe wa Papa 2023

China ilikuwa kituo cha nne na cha mwisho cha mjumbe wa Papa ambaye kati ya Juni na Julai  mwaka huo huo alitembelea kwanza Kiev, kisha Moscow nchini Urusi na baadaye Washington, Marekani kwa lengo la “kupunguza mvutano katika mgogoro wa Ukraine, kwa matumaini, ambayo Baba Mtakatifu hawezi kutupilia mbali, kwamba hii inaweza kuanzisha njia za amani.” Kisha mnamo Septemba 2023 kwa siku tatu Kardinali Zuppi alitembelea katika mji mkuu wa China, ambapo alikuwa na mazungumzo na Li Hui na Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Watu wa China juu ya vita vya Ukraine na haja ya kuunganisha jitihada za kuhimiza mazungumzo na kutafuta njia ambazo kusababisha amani. Hitaji hilo pia ndilo lilirejewa katika simu iliyopigwa.

Kardinali Zuppia azungumza na Li
17 August 2024, 12:50