Tanzania:Toleo la II la mashindano ya Kombe la Zanzibar la kitesurfing Agosti,24!
Pope
Waandaaji wa mashindano yanayotarajiwa ya Zanzibar Cup waliliwasilisha tukio la mchezo wa kitesurfing katika mkutano na waandishi wa habari mjini Zanzibar siku ya Ijumaa tarehe 16 Agosti 2024. Kamisheni ya Utalii Zanzibar na Baraza la Michezo la Taifa la Zanzibar alilitangaza tukio la pili la aina hiyo lililoitwa rasmi “Zanzibar CUP KUSI 2024” huku ‘Kusi’ likimaanisha jina la upepo wa msimu katika ukanda huo wa Tanzania na kufanya mchezo wa kitesurfing kufanikiwa.
Mashindano ya kitesurfing yamepangwa kufanyika Jumamosi tarehe 24 Agosti 2024, hali ya hewa ikiruhusu, huko Kiwengwa katika mkoa wa Kaskazini Unguja Zanzibar. Hii ni ishara ya Pili ya Kimataifa ya Kitesurfing Regatta, mchezo maarufu sana wa Zanzibar unaojulikana kwa asili yake wa kushangaza, katika fukwe, na mandhari nzuri ya pwani hiyo. Kufikia sasa washiriki 33 wamesajiliwa, wakiwemo wachezaji wanne wa kitaalamu kutoka Austria, Italia, Afrika Kusini na Uingereza. Washiriki wengine waliowakilishwa wanatoka Poland, Jamhuri ya Czech, Hispania, na baadhi ni Watanzania.
Anayeratibu shindano hili la Pili la kimataifa ni daktari Stefano Conte, kutoka Italia, mkaazi wa Zanzibar na mpenda mchezo wa kitesurfing. Dk. Conte ni daktari wa upasuaji wa watoto ambaye amejitolea utaalamu wake kwa miaka mingi barani Afrika.
Pia alisaidia kuandaa michuano ya kwanza ya Kombe la Zanzibar iliyofanyika mwezi Februari 2024, wakati katika mahojiano na Pope, alieleza kuwa “lengo ni kuunda mkutano wa watu katika ardhi ya Afrika, watu mbalimbali kutoka pande zote za ulimwengu, wakiwa wameungana katika shauku yao ya mchezo mmoja. Tukio hili kwa njia mbalimbali linawakilisha ujumbe wa amani.”
Kwa njia hiyo Wadhamini wa shindano la mwezi Agosti ni pamoja na Kamisheni ya Utalii ya Zanzibar na baadhi ya hoteli na wafanyabiashara wa ndani ambao watasaidia kwa malazi na huduma kwa washiriki na wajumbe. Zanzibar, visiwani karibu na pwani ya Tanzania, pia inalenga kuongeza utalii wa michezo katika eneo hilo ili liwe aina ya kitovu cha michezo katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.