Serikali ya Nicaragua imevunja asasi za kiraia nyingine 169
Pope
Ufungaji mpya wa mashirika yasiyo ya kiserikali ulitolewa hivi karibuni nchini Nicaragua, baada ya serikali ya Rais Daniel Ortega kufuta hadhi ya kisheria ya taasisi 169 zisizo za faida zinazofanya kazi nchini humo. Siku kumi na moja zilizopita, utaratibu kama huo huo ulifanyika dhidi ya Mashirika hayo yasiyo ya kiseikali (NGO) mengine 1,500. Hii inafanya kuwa jumla ya mashirika ya kiraia yaliyopigwa marufuku tangu kuanza kwa maandamano dhidi ya serikali mwaka 2018 kufikia zaidi ya 5,600.
Wajibu wa kushirikiana na Serikali
Ikiwa hadi sasa hatua hizi za ukandamizaji zimetekelezwa dhidi ya taasisi za Kanisa Katoliki, tovuti huru zinaripoti kwamba wakati huu wale ambao wameathiriwa wako juu ya mashirika yote ya kiinjili, Wapentekoste na Wabaptisti, na mashirika kama vile Save the Children Canada. Kwa ujumla, mashirika hayo yanashutumiwa kwa kutoweka wazi bajeti zao na kubadilisha fedha ili kudhoofisha utawala wa Sandinista. Kuanzia sasa, kwa hiyo, wakitaka kuendelea kufanya kazi watalazimika kufanya hivyo kwa ushirikiano wa karibu na vyombo vya dola na serikali.
Marekebisho ya Kanuni ya Jinai
Rais Ortega, katika muhula wake wa nne mfululizo katika nchi hiyo ya Amerika ya Kati, pia alituma muswada kwenye Bunge la Kitaifa ambao unalenga kurekebisha Kanuni ya Adhabu, akiongeza, miongoni mwa mambo mengine, uhalifu wa ufadhili wa ugaidi, uhalifu dhidi ya utawala wa umma, uhalifu dhidi ya serikali.au taasisi zake na uhalifu wa kompyuta. Hadi sasa haya ndiyo yamekuwa mashitaka ya mara kwa mara yanayotumiwa na serikali dhidi ya wapinzani wake na kutaifisha mali za taasisi mbalimbali japokuwa hazijaainishwa wazi katika Kanuni ya Adhabu. Mpango wa Ortega pia unalenga kurekebisha kifungu cha 410, ambacho kinaadhibu watu au taasisi zinazodhoofisha uadilifu wa kitaifa, kwa kuongeza kutoka miaka 15 hadi 30 jela kwa wale wanaopanga, kufadhili au kufadhili uhalifu huo kwa njia yoyote. Marekebisho ya kanuni ya adhabu yanalenga kupanua kanuni ya utendakazi wa uhalifu ulimwenguni kote ili uhalifu huu uweze kuhusishwa na Wanicaragua au wageni, moja kwa moja au kupitia Mashirika yasiyo ya kiserikali(NGO,) hata ikiwa inafanywa nje ya eneo la kitaifa. Zaidi ya hayo, hukumu ya makosa makubwa zaidi inaweza kuongezwa hadi kifungo cha maisha.