蜜桃交友

Tafuta

Kila siku ni maujai huko Kivu Kaskazini mwa Congo. Kila siku ni maujai huko Kivu Kaskazini mwa Congo.  (AFP or licensors)

Congo:mauaji mapya huko mashariki mwa Congo kwa mikono ya kijihadi wa ADF

Kwa mujibu wa takwimu rasimi zilizowakilishwa tarehe 10 Juni 2024 na Serikali ya Congo(DRC)kati ya mfululizo wa mashambulizi yaliyotokea tarehe 7 Juni na wanamgambo wa ADF katika Eneo la Ben,Kaskazini mwa Kivu,Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ni 41.Wakati huo huo Watoto ni waathirika wakubwa wa ukiukaji katika mauji kulingana na taarifa za UNHCR.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ni watu 41 waliouawa kwa mujibu wa takwimu rasimi zilizowakilishwa tarehe 10 Juni 2024 na Serikali ya Congo DRC kati ya mfululizo wa mashambulizi yaliyotokea tarehe 7 Juni na wanamgambo wa ADF katika Eneo la Ben, Kaskazini mwa Kivu, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Kwa mujibu wa Serikali ya Kinsahasa, watu 39 waliuawa katika vijiji vya Masala, Mahibi vinegne viwili vya Keme. Na watu zaidi ya 9 wamebaki majeruhi. Vikosi vya Muungano wa kidokrasia (ADF) ni kikundi asili cha Uganda ambacho kwa makumu ya miaka kimejibamiza huko Mashariki wa DRC kwa namna ya pekee kaskazini mwa Kivu.

Kunako mwaka 2019 ADF ilijiandikisha kwa Serikali  ya Kiislamu kwa kusisitiza wasifu wao wa kijihadi. Mauaji ya mwisho yaliyotekelezwa ( yaliyotanguliwa zaidi ya watu 15 waliuawa tarehe 4 Juni 2024 huko Masau, mpakani kati ya Wilya ya Kivu Kaskazini na Ituri, wakati zaidi ya mauaji ya wingi yaliyotokea mwezi Aprili na Mei) ya kutatanisha  inaonekana kuwa ni kutokana na operesheni ya Shujaa, iliyoendeshwa kwa pamoja na majeshi ya Congo na Uganda kuwasaka wanajihadi wa ADF. Operesheni iliyoanzishwa mnamo Septemba 2021, hata hivyo, ilisababisha harakati kuelekea magharibi ya wanachama wa ADF ambao, kuwatoroka wanajeshi wa Congo na Uganda, wanaelekea Mangina na eneo la Mambasa huko Ituri. Katika maeneo haya ADF inalenga kupora rasilimali za ndani kama vile kakao na kunyonya migodi ya kienyeji ili kujipanga upya na kuendelea na vitendo vyao vya kuua.

Watoto kuwa waathirika wakubwa katika maeneo ya vita DRC

Mbali na mauaji, watoto wamekuwa ni waathirika wakubwa wa utekaji nyara, unyanyasaji wa kingono, lakini pia kuandikishwa na kutumiwa na makundi yenye silaha vitani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC. Limesema hayo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR tarehe 10 Juni 2024 huku likibainisha kuwa dhuluma nyingi dhidi ya watoto hao huko Kivu Kaskazini hutokea katika maeneo ya mapigano. Kulingana na UNHCR, kesi 164 za ukiukwaji wa haki za watoto ziliripotiwa mwezi Mei, ambapo zaidi ya nusu zikiwa ni kesi 91 zilikuwa ni za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Ripoti hiyo ya hali ya watoto ya UNHCR inabainisha kesi za mauaji na ukeketaji wa watoto kuwa ni asilimia 36, vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa dhidi ya watoto ni asilimia 25, kuandikishwa na kutumia watoto vitani asilimia 18, na utekaji nyara wa watoto ni asilimia 19.

Vitendo vingi vya ukiukaji huu mkubwa kwa asilimia 87 ulirekodiwa katika maeneo ya mapigano, wakati wa uondoaji wa wahusika waliohusika katika vita au katika maeneo yanayodhibitiwa na vikundi vyenye silaha.  "Maeneo haya yameshuhudia ongezeko la mauaji ya watoto kwa mabomu na unyanyasaji wa kijinsia na kuajiriwa jeshini, hasa katika eneo la Nyiragongo," ameeleza kwa kina Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa shirika la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR Filippo Grandi katika ripoti yake. Kwa taarifa hiyo ya UNHCR inaonyesha kwamba huko Beni, watoto walidaiwa kutekwa nyara na kundi la Allied Democratic Forces ADF wakati wa mashambulizi mbalimbali. Huko Nyiragongo, kuandikishwa na kutumiwa kwa baadhi ya watoto katika kundi lenye silaha kulibainishwa. “Eneo la Rutshuru, vikundi vya Mutanda, Bishusha, Bambu, Kihondo na Kanyabayonga viliathirika na mauaji na ukeketaji wa watoto, utekaji nyara na vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa dhidi ya watoto katika mazingira ya mapigano na kulipiza kisasi.”

Shirika hilo la wakimbizi limekumbusha kuwa Umoja wa Mataifa ulithibitisha zaidi ya vitendo 1000 vya ukiukwaji mkubwa dhidi ya watoto katika majimbo matatu ya Mashariki mwa DRC ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini katika robo ya kwanza ya mwaka huu.  Hili linawakilisha ongezeko la 30% kutoka robo ya mwisho ya 2023, na uajiri na utumiaji wa watoto vitani ukiwa umeenea zaidi. Mwezi Aprili 2024 pekee, zaidi ya vitendo 450 vya ukiukwaji dhidi ya watoto vilithibitishwa kote mashariki mwa nchi hiyo. Zaidi ya hayo, unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto uliendelea kuwa juu mwaka 2023 na kuongezeka zaidi mwaka 2024.  Mwezi Mei, kesi 150 za ukatili wa kijinsia GBV, zilirekodiwa, ambapo zaidi ya robo tatu ambazo ni kesi 114 zilikuwa za ubakaji. Kwa mujibu wa UNHCR kwa kiasi kikubwa ubakaji huu 97% ulifanyika katika maeneo yaliyoondolewa wanamgambo wenye silaha na mapigano huko Masisi, Rutshuru, na vile vile katika maeneo yanayohifadhi wakimbizi wa ndani huko Goma na Nyiragongo.

Kesi mbaya zaidi za GBV zilibainika hasa katika maeneo ya Mweso, Nyiragongo, Kirotshe, Kibirizi na Katoyi. Kwa upana zaidi, tathimini ya ulinzi imeorodhesha zaidi ya vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu 1,400 katika jimbo la Kivu Kaskazini.  Watu waliorejea na waliokimbia makazi yao ambao ni wakimbizi wa ndani wanasalia kuathirika zaidi na ukiukaji huu.  Kwa mujibu wa tathimini maeneo yaliyoathirika zaidi ni Masisi, Beni na Rutshuru. Umoja wa Mataifa, unasema hili ni ongezeko la karibu 5% ya ukiukaji na unyanyasaji tangu mwezi Aprili.  

Ongezeko hili linaweza kuhusishwa na kuendelea kwa mapigano kati ya kundi la M23, vikundi vingine vyenye silaha na vikosi vya wanajeshi vya DRC (FARDC) katika maeneo ya kusini mashariki mwa Masisi na kaskazini mwa Rutshuru. Mapigano haya yalisababisha watu wengi kuhama makazi yao, haswa kuelekea kusini mwa Lubero. Matukio haya ya hivi karibuni yanakuja huku kukiwa na kuendelea kwa mapigano mashariki mwa DRC, hasa mapigano kati ya M23, makundi mengine yenye silaha na FARDC.  "Mapigano haya yalikaribia mji wa Kanyabayonga na kusababisha watu wengi kuhama makazi yao na ukiukwaji wa haki za binadamu," limehitimisha shirika la UNHCR.

11 June 2024, 10:35