蜜桃交友

Tafuta

Kanisa Katoliki la Nicaragua lilifanya Juma takatifu bila  maandamano mitaani. Kanisa Katoliki la Nicaragua lilifanya Juma takatifu bila maandamano mitaani.  (ANSA)

Nicaragua,wachungaji 11 wa kiinjili watiwa mbaroni

Wachungaji wanaohusishwa na shirika la Kiinjili liitwalo Mountain Gateway la Marekani,walikamatwa miezi 2 iliyopita na kuzuiliwa kuwasiliana na wanasheria au wanafamilia.Baada ya kusikilizwa kesi ya siri,sheria iliwatia hatiani kwa mashtaka ya uchakachuaji fedha.Hukumu ni kati ya miaka 12 na 15 jela na faini ya dola milioni 80 kwa kila mtu.

Osservatore Romano

Wachungaji 11 wa Kiinjili wanaohusishwa na shirika la Mountain Gateway nchini Marekani la wametiwa mbaroni na mahakama ya Nicaragua kwa tuhuma za uchakachuaji wa fedha. Kwa wanachama wa shirika lenye makao yake huko Texas - walikamatwa miezi miwili iliyopita na kuzuiliwa katika kifungo cha upweke bila kuwasiliana na wanasheria au wanafamilia na hivyo  majaji walitoa hukumu za kati ya miaka 12 na 15 jela, pamoja na faini ya dola milioni 80 kwa kila mtu.

Kesi ilifanyika nyuma ya milango iliyofungwa. Hii iliripotiwa na shirika la Kutetea uhuru (Alliance in Defense of Freedom, Adf Internacional,) ambalo lilizungumzia hukumu isiyo ya kawaida kutokana na kesi ambapo mamlaka hazikuweza kuwasilisha ushahidi wowote. ADF imeomba kuingilia kati kwa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu kwa kutaka mamlaka ya Managua dhamana ya heshima kwa wafungwa wakati wa kukaa gerezani.

Wakati huo huo, kwa mwaka wa pili mfululizo, katika Juma Takatifu ilifanyika Nicaragua bila maandamano katika mitaa ya miji na Njia ya Msalaba kwani yalipigwa marufuku na mamlaka. Shughuli pekee zilizoidhinishwa zilifanyika ndani ya mahali pa ibada au katika maeneo yao. Maafisa elfu nne wa polisi walipangwa kuzunguka makanisa nchini ili kuhakikisha kwamba marufuku hiyo imefuatwa kikamilifu.

04 April 2024, 15:23