蜜桃交友

Tafuta

Hali nchini Sudan ni mbaya sana. Hali nchini Sudan ni mbaya sana.  (AFP or licensors)

Sudan:kusubiri kwa uchovu na hali ya hatari kwa wakimbizi

Wito ulizinduliwa na vyanzo vya ndani kwa shirika la Habari za Kimisionari la Fides kuwa hali katika kambi imezorota na ni ngumu kupata chakula, huduma za afya karibu hazipo na wagonjwa wanateseka sana na hakuna shule.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Huduma muhimu zaidi hazipo, wakimbizi katika kambi ya Gorom, magharibi mwa Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, wanatatizika kupata chakula. Huu ndio wito uliozinduliwa kwa shirika la Habari za Kipimisionari (Fides) na chanzo cha ndani kuhusu kuzorota kwa hali na matatizo makubwa ya kambi moja nchini. Wakimbizi wanatatizika kupata chakula kwani Mashirika ya misaada ya kibinadamu hutumia dola 8 kwa kila mtu kwa mwezi, ambayo inatosha kwa mlo mmoja tu kwa siku.”

Dharura ya afya na elimu

Huduma za afya karibu hazipo na wale walio na hali sugu za kiafya hujikuta wakikabiliwa na mateso makubwa. Kituo cha matibabu cha kambi hiyo kinatarajiwa kuhudumia watu 2,000, wakati kambi hiyo kwa sasa inahifadhi zaidi ya wakimbizi 18,000 ikiwa na daktari mmoja tu wa maabara. Baadhi ya wagonjwa wanahamishiwa katika hospitali ya Juba, lakini wanapata shida kupata matibabu kwa sababu hawawezi kulipia. Sekta nyingine iliyoadhibiwa kabisa ni elimu, huko Gorom hakuna shule za msingi na shule moja tu ya sekondari, lakini hadi sasa wanafunzi wa Sudan hawajakubaliwa. Serikali inasimama upande wa wakimbizi, lakini haina uwezo au rasilimali za kuwapatia huduma na usaidizi.

Zaidi ya watu elfu 4 wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa mahitaji ya kimsingi

Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), lililotajwa tena na  Shirika la habari za Kimisionari (Fides), hadi kufikia tarehe 4 Februari 2024 kulikuwa na watu 542,199 waliokimbia vita nchini Sudan, ambavyo vimedumu kwa zaidi ya miezi kumi, kuelekea Sudan Kusini. Takriban thuluthi moja kati yao ni Wasudan, 80% ni raia wasio Wasudan, wengi wao wakiwa wakimbizi wa Sudan Kusini. Zaidi ya hayo, onyo la janga la kibinadamu linalokaribia kutishia maisha ya maelfu ya wakimbizi wa Sudan nchini Sudan Kusini lilitolewa na shirika la Youth for Darfur Mashad. Walisema kuwa zaidi ya watu elfu 4 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa mahitaji ya kimsingi. “Ukimya wa mashirika mengi ya kimataifa ya kibinadamu kuhusu utoaji wa misaada unawakilisha hatari kubwa kwa wakimbizi wa Sudan nchini Sudan Kusini, ambayo inaweza kusababisha kuzorota kwa hali ya maisha katika kambi ambazo tayari zinakabiliwa na ukosefu wa chakula na dawa.!

Nchini Sudan Kusini karibu watu 1,500 waliokimbia makazi kwa siku

Wakimbizi wa Sudan wanakabiliwa na kusubiri kwa nguvu katika kambi zilizo na msongamano mkubwa wa Sudan Kusini. Wengi hutumia miezi kadhaa katika kambi za wasafiri, wakitumaini kurejea nyumbani hivi karibuni. Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, karibu watu 1,500 waliokimbia makazi yao kutokana na mzozo huo wanafika Sudan Kusini kila siku, na tangu mwanzo karibu watu milioni nane, nusu yao wakiwa watoto, wameikimbia nchi hiyo. Zaidi ya hayo, karibu watu milioni 25, zaidi ya nusu ya wakazi wa Sudan, wanahitaji msaada wa kibinadamu, wakati wastani wa watoto milioni 3.8 chini ya miaka 5 wanakabiliwa na utapiamlo.  

[ Audio Embed WATU WANATESEKA NCHINI SUDAN ]                           

22 February 2024, 15:58