蜜桃交友

Tafuta

2025.01.14 Kardinali Parolini na Mabalozi wa Vatican wa Mashariki ya Kati. 2025.01.14 Kardinali Parolini na Mabalozi wa Vatican wa Mashariki ya Kati. 

Kardinali Parolin akutana na mabalozi wa Mashariki na kuzungumza na rais mpya wa Lebanon

Taarifa kutoka Vatican inafahamisha kwamba Katibu wa Vatican alikuwa na mkutano huko Amman na wawakilishi wa Papa wa Bahrain,Misri,Falme za Kiarabu,Jordan,Iran Iraq, Israel,Kuwait,Lebanon,Oman,Palestina,Qatar,Syria na Yemen.Usitishwaji wa mapigano ulitarajiwa katika nyanja zote na hamu ya amani katika Mashariki ya Kati.Katika mazungumzo ya simu na Aoun,amemtakia heri kwa kuchaguliwa.

Vatican.

Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatica alizungumza na Rais wa Lebanon SuaJoseph Aoun, Jumatatu alasiri, 13 Januari 2025. Katika mazungumzo yao Kardinali alimpongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri hiyo na kuelezea matashi mema huku akimwakikishia sala zake. Pia alibainisha kwa furaha ya kuteuliwa kwa wakati kwa Bwana Nawaf Salam kama Waziri Mkuu tarehe 13 Januari. Akiwa huko Amman, nchini Yordan alikokwenda kwa ajili ya kutabaruku Kanisa la Ubatizo wa Yesu, Kardinali Pietro Parolin  Januari 13 aliongoza mkutano wa Mabalozi wa Vatican katika eneo la Mashariki ya Kati. Hayo yalitangazwa katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka mjini Vatican, ikibainisha kwamba mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa Papa walioidhinishwa katika Ufalme wa Bahrain, Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, Umoja wa Falme za Kiarabu, Ufalme wa Hashemite wa Jordan, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Jamhuri ya Iraq, Serikali ya Israel, Serikali ya Kuwait, Jamhuri ya Lebanon, Usultani wa Oman, Serikali Palestina, Serikali ya Qatar, Jamhuri ya Kiarabu ya Syria na Jamhuri ya Yemen.

Kanisa la Ubatizo nchini Yordan lililotabarukiwa na Kardinali Parolin
Kanisa la Ubatizo nchini Yordan lililotabarukiwa na Kardinali Parolin

Taarifa  hiyo inaeleza kuwa “Katika mkutano huo, migogoro inayoendelea hivi sasa katika eneo hilo ilishughulikiwa, hali ya kisiasa na kikanisa ya kila nchi, ishara za matumaini ambazo zinaweza kuonekana katika baadhi, hali mbaya ya kibinadamu ambayo watu walio hatarini zaidi. kujikuta wanahusika katika migogoro, hitaji la mshikamano kutoka kwa jumuiya ya kimataifa." "Ilitarajiwa vita viweze kukoma hivi karibuni katika pande zote na Mashariki ya Kati inaweza kuwa nchi ya amani, ambapo Wakristo wanabaki kuwa sehemu muhimu ya kuishi pamoja kidugu kati ya dini mbalimbali na kwa maendeleo ya Vijiji vyao."

Kardinali Parolin na Kanisa la Mashariki ya Kati
Kardinali Parolin na Kanisa la Mashariki ya Kati

Piga simu na rais mpya aliyechaguliwa wa Lebanon

Wakati huo huo, Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican ilitangaza kwamba tarehe 13 Januari 2025   Kardinali Parolin alizungumza Joseph Aoun, Rais wa Lebanon aliyechaguliwa Januari 9 iliyopita 2025.   Wakati wa mazungumzo ya simu, Kardinali alimpongeza kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Jamhuri na akatoa salamu za rambi rambi, akimhakikishia maombi yake. Pia alionesha furaha ya uteuzi ufaao kwa Waziri Mkuu Bwana Nawaf Salam uliofanyika tarehe 13 Januari 2025.

Kardinali Parolin akiwa Yordan
14 January 2025, 16:54